Zoezi la sense wilayani Kibondo watu wakamatwa kwa kugoma huku DC Mwamoto akipita kuhamasisha wananchi wajitokeze kuhesabiwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, August 30, 2012

Zoezi la sense wilayani Kibondo watu wakamatwa kwa kugoma huku DC Mwamoto akipita kuhamasisha wananchi wajitokeze kuhesabiwa.


Mkuu wa wilaya ya kibondo Bw Venance Mwamoto (kushoto) akiangalia dodoso zilizochanwa na makarani wa sensa ya watu na makazi (picha na James Jovin )


Watu wawili makarani wa sensa wilayani Kibondo mkoani Kigoma wanashikiliwa na jeshi la polisi wakituhumiwa kuchana dodoso za sensa ya watu na makazi inayoendelea kwa sasa nchini.


Jeshi la polisi limesema kuwa makarani hao ni pamoja na  Elisha Claudias ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu dodoma pamoja na Fredrick Mhalafu mkazi wa Kibondo mjini. 


Mkuu wa wilaya ya kibondo Bw Venance Mwamoto ambaye pia aliongozana na mkuu wa jeshi la polisi Bw Marko Joshua amewataka makarani kuendelea na zoezi la sensa na kuwahakikishia kuwa watalipwa posho yao yote.




Mkuu wa wilaya ya kibondo Venance Mwamoto akimpa mama mwenye watoto mapacha aliyekuwa amekataa kuhesabiwa zawadi ya shilingi elfu 10 ya kukubali kkuhesabiwa na makarani wa sensa

Jeshi la polisi wilayani Kibondo  limesema kuwa Elisha alichana dodoso alizokuwa ameshika Fredrick katika kituo walichopangiwa cha Kifura shule ya msingi katika tarafa ya Kifura kata ya Busunzu wilayani kibondo. 


Aidha tukio hilo lililotokea Jumatatu August 26 huko kifura wakati vijana hao pamoja na makarani wenzao wakijaribu kushinikiza kulipwa posho zao baada ya kuletewa posho nusu kinyume na makubaliano yao.



Mkazi wa kifura Kibondo Issa Jumma akiwa kwenye gari la polisi tayari kwa kupelekwa mahabusu baada ya kugoma kata kata kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi.

 Makarani hao wa sensa ya watu na makazi wanashikiliwa na jeshi la polisi wilayani Kibondo kwa uchunguzi zaidi wa tukio hilo ambapo pia limewataka makarani kuendelea na zoezi la sensa na kutochana madodoso kwa kuwa ni kosa kisheria .


Mama huyo anatoka katika familia ya bw issa juma mkazi wa busunzu kibondo ambapo yeye pamoja na kaya nyingine tatu waligoma kuhesabiwa kutokana na maadili ya dini zao (picha na James Jovin).

Chanzo:jamesjovin.blogspot.com
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad